Marekani yafungua mipaka Mexico, Canada

0
84

NEW YORK, Marekani

MAREKANI imefungua mipaka yake inayoiunganisha na Mexico na Canada, hivyo raia waliopata chanjo ya Corona kutoka nchi mbili hizo wataingia na kutoka kuanzia Novemba, mwaka huu.

Inafahamika kuwa Marekani iliacha kupokea wasafiri wanaotumia ardhi na vivuko kutoka Mexico na Canada tangu Machi, mwaka jana, sababu kubwa ikiwa ni kuzuia kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

Hata hivyo, bado Marekani imeendelea kuwawekea ngumu wasafiri wasio raia wa Marekani wanaotokea Uingereza, China, India, Afrika Kusini, Iran, na Brazil.

Wiki iliyopita, Kituo cha Kuzuia na Kukabiliana na Magonjwa nchini Marekani ilieleza kuwa wasafiri wote wanaoingia lazima wawe wamepata chanjo ya Corona inayotambuliwa na Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) na Taasisi yake ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (FDA).

Source: mtanzania.co.tz